24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Array

NGOs zapewa onyo na siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu

-Mwanza

BODI ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs), imeyatahadharisha mashirika yasiyo ya kiserikali kutojihususha na masuala ya kisiasa bali wasimamie katiba zao katika kutekeleza majukumu ya kuisadida jamii ya Watanzania.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk Richard Sambaiga, alitoa tahadhari hiyo mkoani Mwanza alipokutana na wadau wa mashirika hayo mara baada ya kutembeea baadhi ya mashiria hayo kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na mashriika ya mkoani Mwanza.

Dk. Sambaiga alisema katika kipindi cha uchaguzi wadau wengi wa NGOs huama katika majukumu yao na kuanza kupeperusha bendera za watu wengine na si kuihudumia jamii inayowazunguka kama katiba zao zinavyoelekeza.

Pia aliwataka wadau wanaofanya kazi za kutoa elimu kwa wapiga kura, kutumia fursa ya Uchaguzi Mkuu ujao kuchangamkia fursa hiyo na kuwataka kutoa elimu ya kupiga kura na si kampeni za kisiasa.

“Kama unaona unataka kujiingiza katika masuala ya kisiasa achana na kazi za NGOs simama wewe kama wewe na sio kuitumia NGOs kwa ajili ya kufanya kampeni au kuwafanyia watu kampeni za kisiasa” alisema Dk. Sambaiga

Dk. Sambaiga alizitaka NGOs kujiendesha kitaasisi na sio kuendesha mashirika hayo kwa maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu bali watekeleze majukumu kwa mujibu wa katiba zao.

“Tumetembelea shirika moja ofisi zipo nyumbani kwa mkurugenzi, tukaomba mikataba ya fedha hana, sasa hili shirika linaendeshwaje na mtu mmoja na lina wajumbe zaidi ya 10”alisema Dk. Sambaiga

Kwa upande wa Msajili wa NGOs, Vickness Mayao, alisema ofisi yake imeamua kutembelea mashirika mkoani Mwanza kufuatilia miradi ianyotekelezwa na mashirka hayo kwa jamii.

“Tumekuja kwenu kwa lengo la kujionea miradi mnayoitekeleza katika jamii na kuona kwa uwazi na uwajibikaji wa mashirika yenu kwa jamii ikiwemo jamii husika  kujua miradi inayotekelewa na gharama zake” alisema Vickness.

MWISHO

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles