31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ngorongoro Heroes kumaliza kazi CECAFA

WINFRIDA MTOI

KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ , leo kinashuka dimbani kuivaa Kenya, katika mchezo wa fainali wa michuano ya Chalenji ya Baraza la Vyama vya Soka kwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), utakaochezwa Uwanja wa Njeru, Uganda.

Hiyo itakuwa mara ya pili kwa  timu hizo kukutana katika michuano hiyo, awali zilikutana hatua ya makundi zikiwa kundi B, ambapo zilifungana mabao 2-2.

Mwenendo huo unaufanya mchezo wa leo kutabiriwa kuwa na ushindani mkubwa.

Zilikotokea  Ngorongoro

Ngorongoro ilizindua kampeni zake kwa kishindo, ikiifunga Ethiopia mabao 4-0, ikatoka sare ya 2-2 na Kenya, kisha ikaipiga Zanzibar mabao 5-0 na kutinga robo fainali

robo fainali, Ngorongoro ilikutana na wenyeji Uganda na kuwachapa mabao 4-2 na kutinga fainali bila kupoteza mchezo.

Kwa upande mwingine, Kenya ilianza harakati zake kwa   kutoa kipigo kikali kwa kuichapa Zanzibar mabao 5-0,  ikaivurumisha Ethiopia mabao 5-0, ikatoka sare ya 2-2 na Ngorongoro na kutinga robo fainali kwa kuiliza Burundi 2-1.

Robo fainali ilikutana na Eritrea na kuibamiza bao 1-0, ushindi ulioipeleka fainali.

Mwenendo wa timu hizo unaonyesha mechi ya fainali  itawakutanisha  wababe wawili, je ni nani anaweza kuibuka na ushindi na kutwaa ubingwa?

Wakizungumzia mechi hiyo, makocha wa timu zote mbili, kila mmoja alikiri ugumu wa mchezo huo kutokana na kujuana vizuri baada ya kukutana hatua ya makundi.

“Tangu hatua ya makundi tumekutana na mechi ngumu, lakini tumepambana, Kenya tutakutana nao mara ya pili, tunajuana hawa ni ndugu zetu, hivyo huu ni mpambano wa ndugu, dakika 90 zitaongea,” alisema Zuberi Katwila kocha Ngorongoro.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Kenya, Stanley Okumbi, alisema timu yake imestahili kufika fainali na anatarajia watakuwa mabingwa.

“Tanzania ina wachezaji wazuri, wamefunga mabao 17, ila kesho(leo) ni fainali, tumejipanga na mbinu za kuwanyamazisha,  tuna nidhamu ya  kushambulia na kulinda,” alisema Okumbi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles