33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

N’Golo Kante aanza mazoezi Chelsea

 LONDON, ENGLAN

HATIMAYE kiungo wa timu ya Chelsea, N’Golo Kante, amerudi na kujiunga na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na kurejea kwa Ligi Kuu England. 

Mchezaji huyo alijiunga na klabu hiyo juzi, lakini alifanya mazoezi ya peke yake kwenye uwanja wa Cobham, huku wachezaji wengine wakiendelea na mazoezi ya pamoja. 

Wachezaji wa timu mbalimbali England waliruhusiwa kuanza mazoezi tangu wiki moja iliopita, lakini mchezaji huyo alikwenda mazoezini na hakuweza kujiunga na wenzake kwa madai kwamba bado ana hofu ya virusi vya corona. 

Kocha wa timu hiyo Frank Lampard, alikubaliana na kauli ya mchezaji huyo kutoungana mapema na wachezaji wenzake kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimesababisha Ligi mbalimbali duniani na shughuli zingine kusimama. 

Hatua hiyo ya mchezaji huyo kurudi mazoezini imekuja mara baada ya wachezaji kufanyiwa vipimo kwa awamu tatu tofauti na kuona hakuna mchezaji wa Chelsea ambaye amekutwa na maambukizi. 

Kante alikuwa na wasiwasi kubwa ya maambukizi ni kutokana na taarifa kwamba watu wenye ngosi nyeusi wanakumbwa kwa urahisi maambukizi ya virusi hivyo vya corona na kupoteza maisha. 

 Hata hivyo hapo awali wachezaji wa timu zote walikuwa wanafanya mazoezi huku wakiwa mbalimbali, lakini kwa sasa wameruhusiwa hata kugusana. 

Ligi hiyo ya England inatarajiwa kurejea Juni 17 mwaka huu wakati huo klabu ya Chelsea ikitarajia kushuka dimbani kwenye mchezo wake wa kwanza Juni 19. 

Wachezaji wengine ambao wamejiunga na klabu ya Chelsea ni pamoja na Christian Pulisic, Mateo Kovacic na Tammy Abraham ambapo walikuwa majeruhi. 

England inaweza kuwa Ligi ya tatu kurejea mapema barani Ulaya baada ya Ujerumani kuwa wa kwanza, wakati huo Ligi Kuu Hispania wakitarajia kurejea Juni 8 na England kufuatia Juni 17. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles