NEYMAR NAHODHA WA KUDUMU BRAZIL

0
957


RIO DE JANEIRO, BRAZIL

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Adenor Bacchi maarufu kwa jina la Tite, amemtaja mshambuliaji wa timu hiyo, Neymar kuwa nahodha wa kudumu.

Kocha huyo amekuwa akibadilisha mara kwa mara unahodha kwa wachezaji wake huku akidai kuwa kufanya hivyo kunasaidia wachezaji kuwa na nidhamu na kujua jinsi ya kujiongoza uwanjani.

Kwa sasa kocha huyo amemtaja Neymar ambaye anakipiga katika klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa kuwa nahodha wa kudumu.

Hata hivyo, mchezaji huyo ameweka wazi kuwa kupewa nafasi hiyo kutamfanya abadilike na kuwa kiongozi bora ndani ya timu.

Neymar ni miongoni mwa wachezaji ambao walitajwa kushindwa kutoa mchango mkubwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi huku timu hiyo ikiondolewa katika hatua ya robo fainali dhidi ya Ubelgiji.

“Nimekubali tena kupewa nafasi hii kwa kuwa nimejifunza vya kutosha na nitaendelea kujifunza zaidi. Jukumu hili ni muhimu sana kwangu,” alisema Naymar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here