27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Neymar kuivaa Colombia

Neymar Junior
Staa wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Junior

FORTALEZA, Brazil

STAA wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Junior, ataichezea nchi yake katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Colombia ambao utachezwa kwenye uwanja wa Estadio Castelao mjini Fortaleza.

Neymar alizua hofu kucheza pambano hilo baada ya kupata maumivu ya goti kwenye mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Chile.

Kwa mujibu wa daktari wa Shirikisho la soka nchini humo (CBF), Jose Luiz Runco alisema kuwa Neymar atakuwa imara kiafya hivyo yupo tayari kwa mchezo dhidi ya Colombia mjini Fortaleza.

Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari alipata wasiwasi juu ya afya ya nyota wake kutokana na mchezo mbaya aliochezewa na Chile.

Baada ya mchezo dhidi ya Chile, Neymar anadaiwa kulalamikia maumivu ya paja la mguu wa kushoto.

“Ni maumivu yake ndiyo kitu kinchotuumiza. Atapumzishwa kwenye mazoezi lakini daktari Runco amesema hakuna sababu za kuhofia kwani atamudu kucheza mechi dhidi ya Colombia,” alisema Rodrigo Paiva msemaji wa CBF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles