23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NETANYAHU: IRAN ITAMILIKI SILAHA ZA NYUKLIA MIAKA 10 IJAYO

YERUSALEM, ISRAEL


WAZIRI Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameonya Iran itamiliki silaha za nyuklia katika miaka 8-10 ijayo, ikiwa hakutakuwa na mabadiliko katika mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa taifa hilo.

Kauli yake hiyo ameitoa siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukataa kuthibitisha mbele ya Bunge ikiwa Iran ilikuwa ikitekeleza sehemu yake ya makubaliano hayo.

Katika mkutano na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu mjini hapa jana, Netanyahu ambaye ni mkosoaji mkuu wa mkataba wa kimataifa wa Iran kuhusu nyuklia, amesema Iran itakuwa na silaha za nyuklia katika miaka 10 ijayo ikiwa mkataba huo hautafanyiwa mabadiliko.

Akikataa kuuthibitisha mkataba wa Iran, Trump alilipa Bunge la Marekani siku 60 kuamua ikiwa vikwazo vilivyoondolewa dhidi ya Iran wakati mkataba huo uliposainiwa vitarudishwa.

Wakati huo huo Rais wa Iran Hassan Rowhani amekaribisha uungwaji mkono wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu mkataba huo, licha ya Rais Trump kuutilia shaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles