Imechapishwa: Mon, Oct 9th, 2017

NELLY ATUHUMIWA KUBAKA

OLYMPIA, WASHINGTON


NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Cornell Haynes ‘Nelly’, ameripotiwa kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kubaka mwanamke kwenye gari yake.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, msanii huyo mwenye umri wa miaka 42, alikuwa kwenye basi lake kwenye ziara ya muziki huko Washington, hivyo msanii huyo alikuwa na mwanamke kwenye gari hiyo na hatimaye kumbaka saa 9 45 usiku.

Msanii huyo na wenzake walikuwa wanatarajia kufanya shoo kwenye tamasha mjini Ridgefield mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini hadi sasa inadaiwa kuwa yupo chini ya ulinzi wa polisi, huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

Mwanasheria wa msanii huyo, Scott Rosenblum, aliweka wazi kuwa mteja wake amekuwa akituhumiwa mara kwa mara na mambo ya kutengenezwa, hivyo hakuna ukweli wowote juu ya tukio hilo.

 

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

NELLY ATUHUMIWA KUBAKA