25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NEC: MATUMIZI YA LESENI KUPIGA KURA PALE PALE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesisitiza matumizi ya pasi ya kusafiria na leseni ya udereva kama vitambulisho mbadala kwa wapiga kura ambao watakuwa wamepoteza vitambulisho vya kupigia kura vilivyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), yako pale pale.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima ametoa ufafanuzi wa suala hilo kutokana na maoni ya watu mbalimbali ambao wameonyesha wasiwasi wao kuhusu matumizi ya vitambulisho hivyo kwamba yanaweza kusababisha udanganyifu katika kupiga kura.

Amesema suala hilo lipo kisheria na lina nia nzuri ya kuboresha na kuwapa wapiga kura fursa ya kushiriki katika uchaguzi na kwamba agizo hilo la tume limetokana na malalamiko ya muda mrefu yanayohoji kwamba ni kwanini tume imekuwa ikiwanyima fursa watu kupiga kura wakati wamendikishwa.

“Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu namba 61 kifungu kidogo cha 3(a) kinaagiza mpiga kura kupiga kura baada ya kuonyesha kitambulisho cha kupiga kura au kitambulisho kingine chochote kadri tume itakavyoelekeza, pia Sheria ya Serikali za Mitaa kifungu namba 62(a) kinaelekeza hivyo hivyo.

“Hao wanaosema kwamba ni goli la mkono haiwezekani kwa kuwa ni lazima vigezo vya majina na picha vifanane na taarifa za mpiga kura zilizopo kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na lazima vizingatiwe. Hatutaruhusu matumizi ya viapo vya mahakama vya kumtambulisha mtu (affidavit),” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Kailima amewaonya wasimamizi wa uchaguzi juu ya matumizi mabaya ya fedha za uchaguzi mdogo wa madiwani wa Kata 43, unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu.

“Fedha za uchaguzi zitumike kwa mujibu wa sheria, isionekane kwamba fedha za uchaguzi ni za kuchezea chezea, hapana, zitumike kwa mujibu wa matumizi ya fedha za serikali. Atakayetumia kinyume na muongozo wa tume, kinyume na sheria ya fedha na kununi za matumizi ya fedha za serikali atawajibika,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles