Ne-Yo hajala nyama miaka miwili

0
417

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Shaffer Smith maarufu kwa jina la Ne-Yo, ameweka wazi kuwa hajala nyama wala vitu vyovyote vinavyotokana na wanyama kwa miaka miwili sasa.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 39, amedai kwa kipindi hicho chote alikuwa anakula vyakula vinavyotokana na mimea huku akiamua kuachana kabisa na suala la nyama na mayai.

“Ninapenda maisha ninayoishi kwa sasa, ni miaka miwili sasa tangu nimebadilisha mfumo wangu wa maisha, sura yangu kwa sasa inanawiri, uzito umepungua kwa kiasi kikubwa,” alisema msanii huyo.

Aliongeza kwa kusema, alifanya maamuzi hayo baada ya kuangailia kipindi cha runinga ambacho kilikuwa kinaonesha ‘afya ni nini’, hivyo kilimfanya achukue maamuzi hayo hasa baada ya kugundua kwamba ulaji wa nyama na mayai kwa wingi unaweza ukasababisha baadhi ya magonjwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here