27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

NDUGAI AWAPIGA ‘STOP’ WABUNGE KUINGIA BUNGENI NA KOPE, KUCHA BANDIA

 
Mwandishi Wetu, Dodoma

Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo amewavunja wabunge mbavu baada ya kupiga marufuku wabunge waliobandika kucha na kope bandia kuingia katika Ukumbi wa Bunge.

Spika Ndugai amesema hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Tawfiq kuhoji idadi ya wanawake walioathirika macho kutokana na matumizi ya kope bandia kwani baadhi ya wanawake wameathirika na vipodozi vikiwamo kucha za na kope za kubandika.

Baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile kujibu swali hilo, Spika Ndugai alisema; “Kutokana na elimu hiyo, na mimi leo napiga marufuku kwa wabunge wote kuingia bungeni wakiwa na kucha na kope bandia, lakini kwa wale wanaojichubua naendelea kuchukua maoni,” amesema Spika Ndugai huku baadhi ya wabunge wanaume wakipza sauti kwa kusema “na nywele bandia huku Dk. Ndunglile akimshukuru kwa kuungana na serikali kupiga marufuku matumizi ya kope na kucha bandia.”

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=63l2-RWFp00[/embedyt]

Aidha, akijibu swali la Fatma, Dk. Ndungulile amesema kwa sasa wizara kupitia Mamlaka Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) haina utaratibu wa kudhibiti kope wala kucha za kubandika kwa sababu hakuna sheria inayoipa ya kudhibiti bidhaa hizo.

“Hivyo basi, kutokana na hilo wizara kupitia TFDA, haina takwimu za kuonesha madhara yaliyotokana na bidhaa hizo kwa kuwa hakuna mfumo wa kupokea taarifa za matumizi ya bidhaa husika,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Ndungulile alisema anaomba kuwapa somo wabunge akisema; “tunapozichubua ngozi zetu tunaondoa kinga, mtu anayejichubua ngozi anaingia katika hatari ya kupata saratani, magonjwa ya ngozi, rangi ya asili ni nzuri ilitengenezwa kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hivyo nawaomba msiharibu ngozi zenu kwa vipodozi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles