26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai awaangukia viongozi wa dini kupinga unyanyapaa

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amewaomba viongozi wa dini nchini kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendeleo kupinga na kukemea vitendo vya ubaguzi na unyanyapaa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (Waviu).

Alitoa kauli hiyo jana jijini hapa wakati wa mkutano wa viongozi wa dini, Serikali na Bunge ambao ndio wameandaa mkutano huo chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Nacopha), kupitia mradi wa Hebu Tuyajenge, kwa msaada wa watu wa Marekani.

Ndugai alisema viongozi wa dini nchini wana nafasi kubwa ya kubadilisha fikra na mawazo ya baadhi ya wananchi kuhusu unyanyapaa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Alisema kuwa unyanyapaa ni moja ya changamoto kubwa iliyopo katika jamii na kuwa viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuweza kuvunja ukimya katika jamii kwa kuelimisha waumini wao.

“Mna nafasi kubwa na ya kipekee kwani viongozi wa dini mnaaminika, mnaheshimika na kusikilizwa katika jamii, hivyo mna uwezo wa kubadilisha jamii waepukane na kuacha tabia ya kunyanyapaa wanaoishi na maambukizi.

“Unyanyapaa ni moja ya mambo yanayotukwaza, sisi tukisema ujumbe unaweza usifike vizuri, lakini viongozi wa dini mna uwezo mkubwa kufikisha ujumbe kwa jamii na kufundisha namna ya kuwafanya waliokata tamaa wapate tumaini jipya na mtaisaidia Serikali katika hili.

“Taasisi za dini mna mafunzo imara ya kupasha habari, kwani tunaamini asilimia 90 ya Watanzania ni waumini wa dini mbalimbali, hivyo tunaomba wakati wa mawaidha au mahubiri yenu hii inaweza kuwa moja ya ajenda na tuna matumaini makubwa na ninyi,” alisema Ndugai.

Alisema kuwa Serikali peke yake haiwezi kupambana na suala la unyanyapaa katika jamii, hivyo wameona wakishirikiana na viongozi wa dini watafikisha ujumbe kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles