25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NDUGAI ATAKA MAWAZIRI KUWAJIBU WAPINZANI KWENYE MITANDAO

 Na ESTHER MBUSSI,DODOMA



Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema imekuwa kawaida kwa wabunge wa upinzani kuchokoza Serikali kwa kuuliza maswali bungeni kisha kutoka nje na baadaye kurusha video zao mitandaoni, hivyo akawataka mawaziri nao kuwafuata huko huko kuwajibu.

Akizungumza bungeni juzi, Ndugai alisema. “Mtaona kuna katabia kana muda sasa ka watu wanachokoza, wanaisema Serikali weee, inapofika muda Serikali kujibu wao ‘wanachimba’, wanatoka humu ndani.

“Wanapotoka humu ndani kuna watu wao tayari wanachukua clip (video) tayari wanarusha kwenye Youtube, Youtube inapoangaliwa nchi nzima, dunia nzima wanaona mawazo yale, utamzuiaje Mtanzania yeyote kuwaamini wale kwamba walichosema ndicho chenyewe?

“Lakini na ninyi upande wa Serikali hakuna clip utakayoiona sijui ya AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) au Profesa Kabudi (Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi) akielezea hayo mambo, hakuna kwa hiyo sasa twendeni kisasa, wanavyoenda wao twendeni hivyo hivyo tuwakute huko huko, eeh na wanafanikiwa sana kuidanganya jamii,” alisema Spika Ndugai.

Katika hatua nyingine, amelifananisha Bunge lake na utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete baada ya wabunge wa Chadema, Halima Mdee na Cecil Mwambe kudai mhimili huo unaingiliwa na Serikali.

Ndugai alisema hata awamu ya Kikwete wabunge hao walikuwa wanaiponda hivyo hata mabunge yajayo watafika mahali na kusema bora lilivyo Bunge la sasa.

Mdee akichangia bungeni juzi, alisema “hili Bunge kwa bahati mbaya na sisi tumezubaa tumeingiliwa, juzi tumeshuhudia Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, (Hawa Ghasia), ambebadilishwa, yeye atasema ameamua…”

Spika alimtaka Mdee kubadilisha kauli hiyo ambayo hata hivyo hakujibu na kuendelea kuchangia akisema.  “Ghasia akiulizwa atasema amejizulu kwa matakwa yake lakini sisi wenye akili tunajua ni kwa sababu alivyosimama na korosho, akaletwa mjumbe mwingine akawekwa pale…” alisema Mdee akikatishwa na Spika ambaye alisema Ghasia alijiuzulu mwenyewe si kwamba ameingiliwa.

Naye Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe, alisema manunuzi ya magari ya mahakama zinazotembea zimetumika bilioni 48, kwa kila gari moja Sh milioni 350, fedha ambazo ni mkpo kutoka Benki ya Dunia (IMF), alisema pamoja na nia ya kutaka kuharakisha haya mambo lakini ndani yake kuna nia ovu  kwamba watu wanataka ‘kupiga dili’ katika ununuzi wa magari hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles