22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

NDUGAI AIBANA SERIKALI MIKOPO KWA WANAFUNZI

Na ESTHER MBUSSI-DODOMA


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameitaka serikali kutoa tamko kuhusu wanafunzi waliokosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kwa Elimu ya Juu (HELSB), kwa sababu ya kukosa fedha za kulipia ada ya usajili chuoni.

Ndugai aliyasema hayo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata (CCM) kuomba mwongozo wa Spika kuhusu wanafunzi hao akisema wanapofika vyuoni wanalipishwa ada ya usajili ili kupata mkopo huo.

“Inashangaza wanafunzi waliodahiliwa wamekosa nafasi ilihali wana sifa lakini pia wengi waliopata nafasi hawajapata mkopo na wakati Rais alisema walio na sifa za kupata mkopo wasisumbuliwe lakini wanasumbuliwa ada ya usajili.

“Ingawa idadi ya wanafunzi wanaopata mkopo imeongezeka lakini wanafunzi wanaopata mkopo ni wachache halafu bado wanapata taabu kuupata, naomba mwongozo wako kuhusu suala hili,” amesema Mlata.

Akijibu, Spika Ndugai alisema jambo hilo ni muhimu likatolewa ufafanuzi kwa sababu si wanafunzi wa mwaka wa kwanza pekee wanaopata madhila hayo.

“Naiomba serikali itoe tamko kesho (leo), haiwezekani mtoto afike chuoni alipie fedha ili apate haki yake ya mkopo.

“Ndiyo maana wamezagaa tu mitaani maskini. Hawa ni watoto wa maskini, naomba kesho saa nne serikali itoe tamko au maelezo ya nini kinaendelea kuhusu watoto hawa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles