27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ndoa yavunjika dakika tatu baada ya harusi

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

UNAWEZA kujiuliza kinachosababisha kutodumu kwa ndoa za siku hizi, na huenda hapo utakuwa unamaanisha zile zizisomaliza mwaka au zaidi ya hapo.

Hata hivyo, kile kilichotokea Kuwait kitakushtua kidogo kwani bibi harusi alirudi kwao na jamaa akabaki ‘msela’ dakika tatu tu baada ya kufunga ndoa.

Hakika hiyo ni zaidi ya ile iliyowahi kuripotiwa mjini Jeddah, Saudi Arabia, ambapo ndoa ilivunjika saa moja baada ya kufungwa, sababu ikielezwa kuwa ni mama na dada wa bwana harusi hawakumtaka mwanamke wake.

Nikirejea kwa hii ya Taiwan, ilikuwa hivi; wakiwa wanatoka mahakamani walikofungia ndoa yao, wawili hao walikuwa wakirudi nyumbani, lakini ghafla mwanamke alikanyaga gauni lake la harusi na kuanguka.

Huku ikitarajiwa kuwa mumewe angempa mkono na kisha safari yao kuendelea, ilikuwa tofauti na huo ndio ukawa mwisho wa kuwa ‘mwili mmoja’ kama walivyoahidi katika kiapo cha ndoa.

Jamaa alionekana kukerwa na kitendo hicho cha bibiye kuanguka na ndipo alipomwita mjinga, kauli iliyomchefua bibi harusi huyo na kusema hataki tena kwenda kuwa mkewe.

Alichokifanya mwanamke huyo ni kurudi nyuma hatua chache kutoka pale mlangoni walipokuwa wamesimama na kumfuata aliyewafungisha ndoa, akimwambia anataka talaka yake.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, ambaye haikuchukua muda mrefu kabla ya kuungwa mkono kila kona na watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter, asingeweza kudumu kuishi na mwanamume wa aina hiyo, kwani kitendo chake hicho kimeonesha wazi kuwa ni mtu asiyejali.

Mmoja kati ya watumiaji wa mtandao wa kijamii aliuunga mkono uamuzi wa mwanamke huyo akisema: “Kama anafanya hivyo mwanzoni tu mwa ndoa, ni bora kuachana naye.”

Mwingine alidakia na kusema: “Ndoa isiyo na heshima mwanzoni tu, ni kama ambayo haipo tu.”

Hata hivyo, suala la talaka limekuwa la kawaida mno nchini Kuwait katika miaka ya hivi karibuni. Hadi mwaka juzi, kiwango cha utoaji talaka nchini humo kilifikia asilimia 60.

Hiyo iliifanya Kuwait ishike nafasi ya sita, sawa na Luxemburg, katika orodha ya nchi zinazoongoza kwa wananchi wake kutwangana talaka, ambapo Ubelgiji bado wanaoongoza wakiwa na wastani wa asilimia 71.

Nchini Kuwait, wadukuzi wa mambo wanasema hilo limechagizwa na sera ya Serikali ya nchi hiyo kutoa msaada wa fedha na mikopo kwa wanaotaka kuoana.

Hatua hiyo ya Serikali ilikuja baada ya utafiti wa mwaka jana kuonesha asilimia kubwa ya wananchi wake hawajaoa au kuolewa.

Sasa basi, inasemekana wengi wamekuwa wakibuni ndoa ili kufaidika na fedha hizo na kisha kuachana na kuoana tena ili kuendelea kuzivuna fedha za serikali.

Nako nchini Taiwan kiliwahikutokea ndoa moja kuvunjika kwa sababu tu mwanamke aliomba talaka kwa kuwa hakujibiwa meseji na mumewe.

Siku hiyo, mwanamke akiwa nyumbani alipata maradhi na ndipo alipochukua simu yake ya mkononi ili kumjulisha mumewe aliyekuwa kazini, akimwambia anakwenda hospitali.

Hata hivyo, bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja uliothibitisha kuwa hata wanandoa hao walioachana dakika tatu baada ya kuoana walifanya hivyo ili kunufaika na fursa hiyo.

Wakati huo huo, vituko vya aina hiyo, ndoa kuvunjika bila sababu za msingi, si tu nchini Kuwait, kwani iliwahi kutokea hata Marekani, ambapo mwanamke aliomba talaka kisa tu alimsikia jamaa huyo aliyeishi naye miaka 22 akisema atampigia kura Rais Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2014.

Katika mlolongo huo wa matukio ya ajabu yaliyowahi kuvunja ndoa, lipo lile la mwanamume mwenye umri wa miaka 99 raia wa Italia aliyempa talaka mkewe aliyedumu naye kwa miaka 70.

Chanzo ni pale alipoikuta barua ya mapenzi aliyoandikiwa mkewe na mwanamume mwingine takribani miaka 50 iliyopita. Katika kuilinda ndoa yake, mwanamke alikiri ni kweli aliyetuma barua kipindi hicho alikuwa mpenzi wake lakini bahati mbaya ni kwamba hilo halikutosha kwa mumewe kuelewa na kuamua kumpa talaka.

Mwaka 2007, mwanamume raia wa Urusi ‘alipoliwa’ katika kamari alimweka rehani mkewe. Huku akifikiri ni siri, taarifa zilimfikia mke, ambaye si tu aliomba talaka, bali pia aliamua kwenda kuishi na mwanamume aliyekuwa akiwekeana dhamana na mumewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles