26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NDALICHAKO AAHIDI UBORESHAJI MIUNDOMBINU MZUMBE

|Mwandishi Wetu, Morogoro



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kuboresha miundombinu katika Shule ya Sekondari ya Mzumbe mjini Morogoro.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo mara baada ya kukagua utekelezaji wa ukarabati wa miundombinu uliokua ukiendelea katika shule hiyo.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo,  Profesa Ndalichako amesema ili kuboresha elimu serikali inaendelea kutatua changamoto za miundombinu na vifaa.

“Wizara yangu itahakikisha inapeleka vifaa vya kutosha vya maabara katika shule hii ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita.

Aidha,  ameitaka shule hiyo kuhakikisha inapandisha ufaulu katika ngazi ya kidato cha nne kama inavyofanya kwa matokei ya kidato cha sita,” amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohammed Utaly amesema Wizara ya Elimu imekuwa ikitoa ushirikiano kwa wilaya katika kuhakikisha elimu inaboreshwa.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Wancleslaus Kihongosi amesema ukarabati wa miundombinu hiyo awamu ya kwanza imehusisha nyumba za walimu 44, mabweni 22, maabara nne, madarasa 19, ukumbi wa mikutano, maabara ya kompyuta na majengo matatu ya utawala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles