28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nchi za Afrika Mashariki kuwasilisha bajeti za mwaka wa fedha 2019/2020.

Mawaziri wa fedha wa nchi za Afrika Mashariki leo Alhamisi Juni 13, wanatarajia kuwasilisha bajeti za serikali za nchi zao kwa mwaka wa fedha 2019/2020.


Kwa upande wa Serikali ya Tanzania inapanga kutumia takriban dola bilioni 14.3 katika mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni ongezeko kutoka shilingi trilioni 32.5 za Kitanzania katika mwaka wa fedha 2017/2018.


Bajeti ya Kenya inakadiriwa kuwa dola bilioni 30.2, ambayo ni kubwa kuliko bajeti zote za nchi nyingine za afrika mashariki kwa pamoja.
Uganda kwa upande wake inakadiria bajeti ya dola bilioni 10.9 huku Rwanda ikikadiriwa kuwa dola bilioni 3.17.


Deni la Kenya limezidi utajiri wake kwa 57%, sehemu kubwa ikitokana na wakopeshaji na wawekezaji wa kimataifa.


Kwa upande mwingine takwimu za madeni ya Rwanda, na Tanzania ni chini ya 40% ya pato jumla nchini.


Wakati mapato yakiendelea kushuka katika mataifa yote ya Afrika mashariki, inatazamiwa kwamba awamu nyingine ya malipo ya kodi na mikopo yataidhinishwa na mawaziri wa fedha katika bajeti ya mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles