26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NCCR wajivunia kuvuna wanachama upinzani

Christina Gauluhanga -Dar es salaam

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimesema hadi sasa kimepokea wanachama wapya 59,680 waliojiunga wakitoka katika mikoa mbalimbali wakiwamo vigogo wa ACT Wazalendo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Anjelina Mutahiwa, alisema NCCR inaendelea na shughuli za kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujiimarisha zaidi.

Alisema wakati wanaendelea na shughuli za chama, wapo wananchi ambao wanaelewa sera za chama na  kuamua kujiunga nao wakiwamo wanachama 9,540  Mkoa wa Mbeya, Shinyanga 20,645 na Kigoma 29,495.

“Mkutano Mkuu wa Taifa ulitoa maagizo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kuandaa mpango kazi kwa mwaka 2020 na ulipitishwa na tunaendelea kufanya shughuli za kukijenga chama,” alisema Anjelina.

Alisema katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi vya siasa wa mwaka 1985 walifanikiwa kupata wabunge 19, lakini kwa sababu ya udhaifu wa uendeshaji chama, uchaguzi wa mwaka 2000 wabunge wote 19 hakuna hata mmoja aliyeweza kurejea bungeni.

Anjelina alisema chama hicho kinaaamini kuwa  kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa, kwa kipindi cha miaka 20 sasa wamejifunza mambo mengi wakiongozwa na itikadi ya utu ambayo ndiyo itikadi bora pekee duniani.

“Tunaomba Watanzania wawapuuze wanaoeneza taarifa ambazo si sahihi kwani chama chetu kinaongozwa  na misingi ya itikadi ambayo ni udugu, maadili, usawa, haki, imani, mabadiliko, uhuru, wajibu, asili, kazi na endelezo,” alisema Anjelina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles