30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NCAA YAWALETA WADAU WA UTALII AICC

Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye Bangu akielezea kuhusu Jukwaa la wadau wa utalii linaloanza kesho AICC Arusha

NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza utekelezaji wa mikakati ya kuongeza idadi ya watalii milioni 2 ifikapo mwaka 2020.

Mikakati hiyo na mambo mengine yanaufanya Uongozi wa NCAA kuwaleta kwenye Jukwaa moja wadau wa utalii ili kujadiliana kwa pamoja masuala mbalimbali ikiwamo maeneo mapya ya uwekezaji.

Akizungumza mjini Arusha Naibu Mhifadhi wa NCAA Asangye Bangu alisema, ili kufikia azma ya watalii milioni 2 wameamua kukutana na kujadili mikakati itakayowezesha kufikia malengo hayo kwa haraka.

“Hivi karibuni tulikuwa na ziara na wawekezaji katika sekta ya utalii wametembelea vivutio na maeneo mapya yanafaa kwa uwekezaji Ngorongoro.

“Tulipokea maoni na mawazo yao hivyo Julai 17, mwaka huu tutakutana na tutakuwa Jukwaa la wadau wa utalii katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa- AICC, mjini Arusha.

“Tumewaalika Chama cha Mawakala wa Utalii (TATO), Kamishana wa Mapato ya ndani TRA, Baraza la Mazingira (NEMC) na wengine ili watuelezee masuala mbalimbali ya kufanikisha jambo hili,” alisema.

Kwa upande wake Katibu wa TATO Cyril Akonai alisema Chama hicho kina wanachama takribani 222 kwa nchi nzima, hivyo wamepanga kushiriki ili kutoa mchango wao katika kufanikisha sekta ya utalii.

Naye Meneja wa Mipango na Uwekezaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Needpeace Wambuya alisema, wanakutana na wawekezaji katika sekta ya utalii ili kupokeza zaidi kutoka kwao.

Jukwaa hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Maliasi na Utalii Japhet Hasunga pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa wa Arusha.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles