25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Natarajia kuiona Simba ya kisasa zaidi

simba_sc-600x400NA BADI MCHOMOLO

NI miaka zaidi ya minne Simba imekuwa na wakati mgumu katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, hii ni kutokana na klabu hiyo kufanya vibaya dhidi ya wapinzani wao, Yanga SC pamoja na Azam FC.

Klabu ya Yanga SC na Azam FC, zimekuwa zikifanya vizuri kutokana na hali yao kiuchumi kuwa sawa japokuwa si sana lakini hauwezi kulinganisha na klabu ya Simba ya sasa.

Hali ya uchumi inaifanya Simba kuyumba hasa katika suala la kufanya usajili kwa wachezaji wenye tija ndani ya klabu ambao wataweza kufanya makubwa katika ushindani wa soka la sasa, japokuwa kulikuwa na udhamini kutoka kwa Kampuni ya Bia (TBL), lakini bado walikuwa na wakati mgumu.

Fedha za wadhamini hao ni wazi kwamba zilikuwa hazitoshi pamoja na kiasi cha klabu yenyewe ambacho wanakipata kwa mwaka kutokana na miundombinu yao.

Kutokana na hali hiyo, mwanachama tajiri wa klabu hiyo, Mohamed Dewji (Mo), ameguswa na kitendo cha Simba kufanya vibaya kwa miaka mingi, hivyo ameweka wazi nia ya kutaka kuwekeza fedha zake kwa ajili ya kurudisha heshima ya klabu hiyo pamoja na kufikiria kutwaa taji la michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa miaka ijayo.

Ni wazo zuri na lenye tija kwa klabu kama hiyo ambayo inakumbwa na ukata wa fedha. Endapo tajiri huyo atapewa timu hiyo basi ni wazi kwamba tunatarajia kuona Simba ya kisasa zaidi baada ya muda mfupi ujao

Mo anataka kuleta mfumo wa hisa katika klabu hiyo ambapo utakuwa ni mpya kwa klabu za soka nchini Tanzania, lakini ndio mfumo ambao wanatumia klabu kubwa ambazo zinashiriki Ligi Kuu nchini England kama vile Manchester United.

United kwa sasa ni klabu pekee ambayo inaongoza kwa utajiri kwa zile ambazo zinashiriki Ligi Kuu, kutokana na makampuni mengi kununua hisa.

Hivyo kwa mipango ya Mo, Simba inaweza kufikia hatua ambayo wengi wetu hatukuwa na uhakika siku moja klabu hiyo itaweza kufika, kikubwa ni kwamba uongozi wa klabu hiyo ubariki ombi la tajiri huyo ili tuweze kuona soka la ushindani kati ya klabu kubwa kama Yanga SC, Simba SC na Azam FC.

Kwa mipango ambayo ameimwaga Mo kwenye taarifa yake na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita, ni wazi kwamba klabu hiyo itakuwa na ndoto za kuliwinda taji la Klabu Bingwa Afrika mbali na Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo linaonekana kuwa ngumu kulichukua kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni dhidi ya wapinzani wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles