24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nape: Serikali haiwezi kufuta michezo

NapeNa RACHEL MRISHO, DODOMA

SERIKALI imesema haiwezi na haina mpango wa kufuta michezo nchini licha ya kufanya vibaya katika mashindano mbalimbali.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Nape alikuwa akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto, aliyehoji ni kwanini Serikali isifute michezo Tanzania?

Alisema nia ya Serikali ni kuiendeleza sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa kwa kuwekeza miundombinu ya michezo na elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Akijibu swali la nyongeza kuhusu ufufuaji wa michezo katika Shule za Msingi na Sekondari ya Umitashumta na Umisseta, alisema Serikali haijafuta michezo hiyo kama inavyodaiwa, bali ilisitisha kwa muda ili kujiandaa na kujipanga upya.

“Michezo ya Umisseta na Umitashumta imekuwa ikifanyika kama matamasha, ikifika kilele hakuna matokeo yanayoendelezwa, hivyo Serikali inajipanga kuhakikisha wanaofanya vizuri wanapelekwa kwenye shule maalumu zinazotengwa kwenye mikoa na wilaya ili kuendeleza vipaji vyao,” alisema Nape.

Akizungumzia suala la uwekezaji kwenye michezo, waziri huyo alisema kama uwekezaji utakuwa mdogo, matokeo mazuri hayawezi kufikiwa.

Aidha, alisema Serikali haijatelekeza michezo hivyo itaendelea kutenga bajeti na kuangalia vyanzo vingine vya kuiendeleza pamoja na fedha zinazotokana na michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa ambazo hufadhili michezo duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles