24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NAPE: NITAFIA CCM

Na AMON MTEGA-SONGEA


MBUNGE wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), amesema kuwa hana mpango wa kuhamia chama chochote cha upinzani na ataendelea kubaki ndani ya CCM.

Alisema hawezi kufanya uamuzi wa kuhamia katika vyama vya upinzani, huku akidai magari ya upinzani kwa sasa yanazidi kuzama.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Songea wakati akimnadi mgombea ubunge wa Songea Mjini kupitia CCM, Dk. Damas Ndumbaro katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Bombambili mjini hapa.

Nape ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM, alisema kama kuna watu walidhani atakihama chama tawala CCM na kujiunga na upinzani wasahau.

Alisema matatizo ya chama humalizwa ndani ya chama na si kukihama kama walivyofanya wanachama wengine waliokimbia ndani ya CCM.

“Naikubali serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na jemedari Dk. John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais na Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Ni serikali yenye viongozi imara na mimi naapa kufia CCM na si vinginevyo.

“Nasikia maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo (jana) watu hao waondokane na mawazo hayo,” alisema Nape.

Pamoja na hali hiyo aliwataka wakazi wa Songea Mjini kutambua kuwa wana kila sababu ya kumchagua Dk. Damas Ndumbaro kuwa mbunge wao kwani ana sifa zote za utumishi kwa wananchi.

Mashambulizi ya kampeni hizo zinazoongozwa na Nape akisaidiwa na mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini, Moses Machali ambaye alijiunga na CCM baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Songea Mjini unatarajiwa kufanyika Januaroi 13, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles