23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nape: Hatumshambulii mtu CCM

kinanaNA ELIYA MBONEA, ARUSHA
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, amesema mawaziri na watendaji wa serikali wanaotajwa kushindwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hawashambuliwi kwa majina yao bali dhamana walizokabidhiwa.
Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa juzi wakati wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema wapo baadhi ya watendaji walioanza kupotosha utendaji wa CCM na masuala yao binafsi.
“Wapo watendaji wa serikali ambao kutokana na utendaji wao kukosolewa wameamua kuligeuza suala hilo kuwa ni vita yao binafsi suala ambalo si kweli, “ alisema Nape na kuongeza:
“Ninawaomba Watanzania mtuelewe, tunapomtaja kiongozi wa Serikali kwamba haendani na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM tunakuwa hatutaji jina la mtu wala kumfuatamfuata mtu tunachokitaja au kukishughulikia ni dhamana aliyopewa na si vinginevyo,” alisema.
Kauli ya Nape imekuja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuashauriwa na CCM kutatua migogoro ya ardhi na mipaka kati ya wananchi na hifadhi za taifa.
Ilielezwa kuwa Nyalandu amekuwa haufanyii kazi ushauri huo badala yake amekuwa akitafuta watu wa kumtetea wakikitaka CCM kisiishambulie wizara yake.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumzia suala la migogoro ya ardhi, alisema Chama kitaendelea kuisimamia Serikali kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Kinana alisema tangu walipoanza kuipigia kelele Serikali, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amefikia uamuzi wa kufuta hati ya matumizi kwenye mashamba saba mkoani Tanga ambayo yatarejeshwa kwa wananchi.
“Uamuzi huo umetokana na ushauri uliotolewa na viongozi wa chama wakati wa ziara iliyofanyika mkoani Tanga na kujionea shida ya ardhi kwa wananchi,” alisema Kinana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles