24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

NAPE MTAKA DK. KILANGI KUISAIDIA SERIKALI KUFUATA SHERIA

Maregesi Paul, Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii, Nape Nnauye amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuisaidia serikali kufanya kazi kwa kufuata sheria.

Nape ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM), ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2018/19 iliyowasilishwa jana na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamis Kigwangalla.

Katika maelezo yake Nape amesema kitendo cha serikali kuamua kufyeka miti katika mbuga ya wanyama ya Selous, hakiwezi kukubaliwa kwa kuwa kinakiuka sheria iliyopitishwa na bunge mwaka 2004.

“Sheria hiyo inataka kabla miti haijakatwa katika maeneo mbalimbali yakuwamo kwenye hifadhi lazima tathmini ya mazingira ifanyike lakini hilo halijafanyika katika mbuga ya Selous ingawa Wakala wa misitu (TFS), wameshatangaza tenda ya kukata miti katika mbuga hiyo kwa ukubwa wa eneo la kama Mkoa wa Dar es Salaam,” amesema.

Kutokana na hali hiyo, Nape ametaka ukataji wa miti huko Selous usimame hadi tathmini itakapokamilika.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema huku akidai ni kwa utani: “ukikata idadi kubwa ya miti katika hifadhi ya Selous huwezi kubaki salama na badala yake utalaaniwa.”

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alisisitiza umuhimu wa mradi huo wa umeme wa Stiggler’s Gorge usimame hadi tathmini ya mazingira itakapokamilika. Kwa mujibu wa zitto kukata miti katika hifadhi ya Selous ni kuharibu mazingira na kwamba hakutakuwa na faida tunayoweza kuipata kupitia mradi wa umeme utakaozalishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles