29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NAMUONA HARMORAPA AKIZIDI KUPEPEA

BADO ni underground, lakini anajulikana! Wengi tumemjua kwa sababu tu anafanana sana na msanii mwingine wa Bongo Fleva, chipukizi anayeelekea kukua, Harmonize.

Harmonize yeye ni msanii anayefanya poa akiwa na Lebo ya WCB, chini ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye uwezo wake na mafanikio yake kwenye muziki huo ni mkubwa na mfano wa wasanii wa Bongo Fleva.

Tumwache Diamond. Huyu Harmorapa amepenyeza kupitia kufanana kwake sura na Harmonize. Wengi walimpuuza na kumuona kama anayebabaika kutaka kupata ujiko kupitia jina la Harmonize.

Pengine inaweza kuwa kweli, lakini vipi uwezo wake kimuziki? Hicho anachosema anacho, kimo ndani yake kweli? Hilo ndilo jambo la kujiuliza.

Binafsi nilianza kumfuatilia Harmorapa baada ya kufurahishwa na vituko vyake. Staili yake ya kiki kiukweli ilinivutia, nikataka kumjua zaidi ni mtu wa namna gani.

Awali nilichokiona kwa Harmorapa ilikuwa ni msanii ama wa komedi au jamaa anayesaka umaarufu kwa njia ya mkato. Nilifikiri hivyo, lakini moyoni nikasema, ngoja nijipe muda kwanza.

Sikutaka kuamini fikra zangu haraka. Nikafuatilia ngoma yake ya ‘Kiboko ya Mabishoo’ aliyomshirikisha mkongwe Juma Nature, nikaona kweli kuna kitu ndani yake, lakini hakikuwa kikubwa sana – nilimuona kama msanii wa kawaida tu, anajitutumia.

Lakini bado nilitaka kumpa nafasi tena ili nijiridhishe kwa mara nyingine kama yeye kweli ni msanii wa Bongo Fleva au komediani.

Nilipokuja kuona kichupa chake cha sasa ‘Nundu’ akiwa amepiga kolabo na C Pwaaa. Aisee acha kabisa. Hapo ndiyo nikamjua vizuri Harmorapa. Jamaa anajua kuimba na ni mbunifu.

Nimetazama kwa makini video ya huo wimbo na kufuatilia mashairi yake na namna anavyotamba akitumia ghani za mafumbo, nikagundua Harmorapa ni aina nyingine kabisa ya wasanii.

Dogo anachana – anaimba Hip Hop ngumu, anateleza na biti na ngoma inachezeka. Ningeendelea kubaki na mawazo yangu ya awali kuwa dogo ni komediani au mtafuta umaarufu kwa njia ya mkato, lakini nimejiridhisha kwamba siyo wa namna hiyo.

Hayo mambo ya kiki, kufanana na Harmonize ni kama sehemu tu ya njia ya kutokea, lakini ndani mwake anacho kipaji.

Hata hivyo anatakiwa kukaza zaidi. Aachane na fikra za kutafuta kiki, tayari zimeshamtoa. Apige kazi tu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles