30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NAIBU SPIKA AMKINGIA KIFUA WAZIRI MKUU KUUJIBIA WARAKA WA KKKT

Na Mwandishi Wetu            |        


Siku moja baada ya Msajili wa Vyama kuiandikia barua Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)  kukanusha waraka walioutoa wakati wa Pasaka, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia ameitaka Serikali kutoa kauli kuhusiana na hilo.

Mbatia ameihoji serikali leo wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, jana msajili wa vyama ameiandikia kanisa la KKKT barua akitaka ifute waraka wake wa pasaka, serikali inatoa kauli gani kuhusiana hilo na ikizingatiwa hawa ni wadau wakubwa wa amani kwa taifa letu na hapo spika ameanza kwa kuomba dua,”amehoji Mbatia.

Kutokana na hilo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amemkia kifua Waziri Mkuu akisema kwamba itakumbukwa kuwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea alihoji kuhusu masuala ya dini lakini Spika Job Ndugai akamwambia waziri mkuu hawezi kujibu masuala ya imani.

“Mtakumbuka kuwa Kubenea aliwahi kuuliza masuala ya dini hapa lakini spika akamwambia kwamba waziri mkuu hawezi kujibu swali hilo kwa kuwa ni suala la imani,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles