29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mwinyi awakumbuka waliofariki Mv Nyerere

Janeth Mushi, Arusha



Rais Mstaafu wa awamu wa pili, Ali Hassan Mwinyi, ametoa rambirambi ya Sh milioni mbili kwa familia za waliopoteza ndugu zao katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani yaliyofanyika kitaifa jijini hapa leo Jumatatu Oktoba Mosi, Rais huyo mstaafu aliwaomba wazee na makundi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo kusimama kwa dakika moja kwa ajili ya kuwakumbuka waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea hivi karibuni na kuua watu zaidi ya 200.

“Tunakutana hapa baada ya janga kubwa lililotokea Ziwa Victoria, waswahili wanasema mkaa na maiti haachi kulia lia nami naanza kwa kutoa milioni mbili kama rambirambi,” amesema Mwinyi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles