33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwingine mbaroni kwa kuchoma juzuu

Oscar Assenga – Tanga

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga , linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Amboni Kata ya Mzizima jiji hapa, Emanuel Kuyanga (49)  kwa tuhuma za kuchoma moto kitabu cha dini ya Kiislamu cha Juzuu.

Tukiom hilo ni la pili kutokea ndani ya wiki moja baada ya mkazi mwingine  ambaye pia ni Ofisa Biashara wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Daniel Maleki aliyedaiwa kuchana kitabu cha dini.

Februari 7, 2020 picha za video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zilimuonyesha Maleki ambaye ni ofisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro akichana kitabu hicho.

Muda mfupi baada ya kusambaa kwa video hizo, alikamatwa na polisi na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kilosa ambako alisomewa mashtaka na kupelekwa mahabusu baada ya polisi kuwasilisha ombi la kutaka asipewe dhamana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Emanuel Minja alithibitisha kukamatwa na mkazi huyo huku akieleza kwamba tukio hilo lilitokea Februari 8, mwaka huu saa mbili usiku.

Alisema kwamba wao walipata taarifa ya tukio la kuchomwa kwa juzuu ambapo walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

Akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa Kaimu Kamanda huyo alisema kwamba nyumbani kwa Emanuel walifika Athumani Rajabu (14) ambaye ni mwanafunzi akiwa na wenzake kwa lengo la kuomba mchango wa maulidi baada ya kufika kwa mtu huyo alitoa juzuu huku watoto hao wakimsihi kutofanya hivyo kwani anaweza kurukwa akili au kuota mkia.

Baada ya mtuhumiwa huyo kusikia maneno hayo, aliagiza kiberiti ndani na kuwapokonya kitabu hicho watoto hao na kisha kukichoma moto.

“Hivyo Jeshi la Polisi kwa sasa linamshikilia Emanuel kwa mahojiano na hatua za kisheria zaidi lakini pia nitoe wito kwa wananchi na wageni kwamba Tanga ni shwari na hakuna migogoro ya kidini,” alisema Kaimu Kamanda

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, alisema kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani leo.

Alisema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi liliwahi kufika kwenye eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa pamoja na mkewe ambao walifikisha polisi Chumbageni kwa usalama wake.

Naye Mwneyekiti Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Khamis Mataka, alisema kuwa tayari Mufti Zubeir ameshatuma ujumbe mkoani Tanga kwa ajili ya tukio hilo.

Kutokana na hli hiyo alilishukuru Jeshi la Polisi kwa hatua ya haraka waliyochukua huku ikiwataka waislamu kuwa subira huku sheria ikiendelea kuchukua mkondo wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles