24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mwingereza ahusishwa Simba

SimbaNA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa timu ya Simba kwa sasa upo kwenye mchakato wa kusaka kocha mkuu mpya baada ya kuachana na Mserbia, Goran Kopunovic, aliyeiongoza timu hiyo kushika nafasi ya tatu Ligi Kuu msimu uliopita.
Habari zilizolifika MTANZANIA jana zimeeleza kuwa Simba ilikuwa kwenye mazungumzo na wakala wa kocha mmoja raia wa England, ambaye jina lake lilifichwa aliyewahi kufanya kazi nchini Afrika Kusini.
“Wakala wake katua nchini juzi (wikiendi iliyopita) na wamefanya naye mazungumzo ili aje kuifundisha Simba msimu ujao,” kilieleza chanzo hicho.
Kilizidi kudokeza kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya viongozi wa timu hiyo kuhusu ujio wa Mwingereza huyo, wapo waliomkubali na wengine kumkataa.
“Bado kuna mvutano baina ya wenye mamlaka ya kupata kocha, kwani baadhi ya viongozi wamesema makocha wa Uingereza hawafanikiwi sana wakija kufanya kazi Afrika, huku wengine wakisema anafaa kutokana na rekodi nzuri,” kiliongeza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe, anayehusika na ujio wa kocha mpya hakutaka kuweka wazi suala hilo na kudai kuwa: “Siwezi nikakutajia jina la kocha ambaye tupo naye kwenye mazungumzo. Kwa sasa tumemtumia mkataba kocha huyo ili auangalie kabla ya kuingia naye makubaliano muda si mrefu tutawajulisha hilo.”
Mbali ya Mwingereza huyo, Simba pia inahusishwa na makocha kadhaa akiwemo kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen.
Simba mpaka sasa imeshasajili wachezaji wanne wapya ambao ni mabeki Samir Haji Nuhu na Mohamed Faki, mshambuliaji Mussa Mgosi na kipa Mohamed Abraham Mohamed, wote hao wamesajiliwa kupitia ripoti aliyoiacha kocha Goran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles