23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwili wa Kibonde wahifadhiwa Bugando

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk. Thomas Rutachunzibwa, amesema mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Kituo cha Radio cha Clouds, Ephraim Kibonde, umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Taarifa iliyotolewa na mganga huyo leo Alhamisi Machi 7, imesema Kibonde alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa katika hospitali hiyo kwa matibabu zaidi.

“Leo Machi 7, saa 11:30 alfajiri hospitali ya Rufaa ya Bugando imepokea mwili wa Ephraim Kibonde, mtangazaji wa Clouds Media,” imesema tarifa hiyo.

Leo saa moja asubuhi, uongozi wa Clouds Media Group, kupitia Mkurugenzi wa Maudhui wa kampuni hiyo, Sebastian Maganga, ulitangaza kifo cha Kibonde ambaye aliugua ghafla baada ya maziko ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba, Bukoba mkoani Kagera juzi na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa huo kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Uhuru jijini Mwanza.

Kibonde amefariki ikiwa ni takribani miezi minane imepita baada ya mkewe Sarah kufariki mwaka jana kwa ugonjwa wa saratani.

Kibonde ameacha watoto watatu, Junior, Hilda na Illaria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles