28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MWIJAGE: ZANZIBAR HAITAIUZIA SUKARI BARA

Ramadhan Hassan, Dodoma


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesisitiza kwamba Zanzibar haitaiuzia  Sukari Tanzania Bara kutokana na kiwanda cha Mahonda kuzalisha tani 4,000 wakati mahitaji yakiwa ni tani 20,000.

Kauli hiyo ameito bungeni jijini Dodoma leo Septemba 7, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Jaku Hashimu Ayoub (CUF).

Katika swali lake ,Jaku alitaka kufahamu ni kwanini Kiwanda cha Mahonda kilichopo Zanzibar kimekuwa hakiuzi sukari Tanzania Bara.

“Naomba Mheshimiwa waziri unisikilize kwa umakini kwa sababu nazungumza Kiswahili, Muungano wetu tumeungana nchi mbili kwa maana Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika ndio maana jina likapatikana Tanzania kati ya mambo tuliyokubaliana katika muungano ni pamoja na ushirikiano katika biashara.

“Sasa ni sababu gani za msingi kiwanda cha Sukari cha Mahonda hata wabunge tumekuwa tukisimama mara nyingi kukizungumzia hapa.Bidhaa zinazotoka Tanzania Bara zinatumika Zanzibar kwanini bidhaa zetu haziwezi kuuzwa Tanzania bara. wakati mwingine zinatumika mpaka bidhaa kutoka nje ya Nchi,” amehoji Jaku.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, akijibu amesisitiza Zanzibar haitaiuzia  Sukari Tanzania Bara kutokana na kiwanda cha Mahonda kuzalisha tani 4,000 wakati mahitaji yakiwa ni tani 20,000 ambapo anawasiliana na watu wa Zanzibar na Waziri wake wa kule kumwambia azalishe auze huko huko Zanzibar.

Kutokana na majibu hayo baadhi ya wabunge walianza kupasa sauti ambapo Mwijage aliendelea kwa kusema kuwa watulie ili awape majibu ya kile walichouliza.
“Mheshimiwa Mwenyekiti kuna wabunge wanataka kujua ninachokisema ningeomba muwape fursa wale wanaotaka kunisikiliza niwaeleze kuhusiana na suala la Mahonda,” amesema

Mwijage amesema amesema kutokana na hali hiyo, alihoji tani nyingine watazitoa wapi. “Mheshimiwa Mwenyekiti tunataka kuondoa usiri katika sukari kwani mafuta ya kula ni siri kwa sababu tunataka kuzalisha ajira na mimi nipo tayari kulisimamia hilo hadi nitakapoambiwa vinginevyo,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles