27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MWIJAGE AANZA KUKAGUA VIWANDA VISIVYOENDELEZWA

Na AGATHA CHARLES

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, amesema yuko katika ziara ya ukaguzi kabla ya kutoa taarifa ya namna atakavyotekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuwanyang’anya viwanda wamiliki walioshindwa kuviendeleza.

Mwijage alitoa kauli hiyo jana kwa njia ya simu, alipotafuwa na MTANZANIA Jumamosi, lililotaka kujua ni lini anaanza rasmi utekelezaji huo na kwamba viwanda hivyo viko maeneo yapi.

“Hivi karibuni nitawaita niwaeleze waandishi, bado nazungukia viwanda, nitawaita niwaeleze,” alisema Mwijage.

Juzi Magufuli akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Pwani, ambako alizindua viwanda saba, alimwagiza Mwijage kuwanyang’anya viwanda  wamiliki walioshindwa kuviendeleza ili wapatiwe wawekezaji wengine.

Katika ziara hiyo, ambako Magufuli aliweka jiwe la msingi katika Kiwanda cha kusindika matunda cha Sayona, kilichopo Mboga, Chalinze, alisema makosa yaliyofanyika ni kuuza viwanda kwa watu binafsi ambako kuna viwanda 197 vimekufa, huku vingine vikiwa magofu.

Tangu wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi na alipoingia madarakani, Magufuli, amekuwa akisisitiza Tanzania ya viwanda na tayari alikwishafanya ziara na kuzindua viwanda sehemu mbalimbali nchini, ikiwamo mkoani Shinyanga, ambako moja ya Kiwanda alichokizindua ni cha kutengeneza mifuko ya sandarusi cha Fresho Investment Company Limited.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles