31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MWIGULU: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAKAZI YA POLISI

 

Na JANETH MUSHI

-ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema serikali itaendelea kuboresha makazi ya Askari Polisi kote nchini.

Mwigulu ametoa kauli hiyo leo jijini Arusha baada ya kutembelea eneo ambalo linajengwa nyumba za askari zilizoteketea kwa moto hivi karibuni ambapo pia amesema hivi sasa katika mikoa saba tofauti hapa nchini ikiwamo Dar Es Salaam, ujenzi wa nyumba za askari unaendelea na ambapo ujenzi wa nyumba hizo utakapokamilika wataangalia namna ya kuboresha na kujenga nyumba nyingine za askari hao kutokana na nyumba wanazoishi sasa kutokuwa na ubora.

Mmoja wa wadau mkoani hapa waliochangia ujenzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzanite One, Hussein Gonga amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa ulinzi na usalama wameamua kushirikiana na serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo.

“Askari wanapaswa kuishi katika mazingira mazuri ili wafanye kazi zao kwa ufanisi, ndiyo maana tumewajibika kwa haraka sana, Rais John Magufuli alitufungulia mlango akatuhamasisha na sisi kama wafanyabiashara tumejitolea kujenga nyumba 18,” amesema.

Gonga amewaomba wadau wengine wakiwamo wafanyabiashara kujitokeza kusaidia ujenzi wa nyumba hizo kwani askari ndiyo wenye jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao hasa ikizingatiwa biashara inahitaji usalama.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya ujenzi,ambaye pia ni mfanyabiashara jijini hapa, Hans Paul ambaye pia anashirikiana na Serikali katika ujenzi huo amesema kwa kutambua umuhimu wa Polisi hasa katika ulinzi na usalama, wameamua kusimamia ujenzi wa nyumba hizo ili polisi hao wapate makazi bora ya kuishi.

“Tunatarajia kutumia zaidi ya ya Sh milioni 400 lakini kwa sababu tukio hilo lilitokea ghafla hatujajua kiasi kitakachotumika hadi nyumba hizo 31 kukamilika kwani tutaweka umeme pamoja na kutengeneza miundombinu ya maji taka,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles