26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwigulu Nchemba asimulia punda walivyosababisha kupata ajali

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, amesema chanzo cha ajali aliyopata ni dereva kukwepa punda watatu.

Ajali hiyo ilitokea leo Jumatano Februari 13, katika eneo la Migori Mkoani Iringa akiwa safarini kuelekea Singida kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya mkoa.

“Punda walikuwa wanavuka barabara sasa dereva wangu akajaribu kuwakwepa lakini ikashindikana, baada ya hapo nilisikia kishindo kikubwa na moshi umetanda ndani ya gari, ilikuwa imepinduka.

“Wasamaria wema wakaja kutuchukua na kutuleta hapa hospitalini, lakini namshukuru Mungu kutoka mzima kwani mkanda ulikuwa umenibana sana,” amesema.  

Mwigulu amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma akiendelea na matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles