MWENYEKITI UVCCM ZIARANI KANDA YA ZIWA

0
965

 

Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAMMwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Kheri James, anatarajiwa kuanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani.

Taarifa iliyotolewa jana na UVCCM ilieleza kwamba ziara ya kiongozi huyo itaanza katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora kuanzia Septemba 20 hadi Oktoba 10.

“Ziara inaanza Septemba 20, itaanza katika mikoa ya  Mwanza, Shinyanga na Tabora hadi Oktoba mwaka huu. Dhumuni la ziara ni kukagua uhai wa chama na jumuiya zake, kuimarisha uhusiano wa chama na Serikali

“Pia kupitia taarifa za utekelezaji wa ilani kwa mambo yanayohusu vijana pamoja na kukagua miradi ya vijana inayowezeshwa na Serikali kupitia halmashauri husika,” ilieleza taarifa hiyo.

Kheri ni mmoja wa viongozi ambao wamekuwa wakisifu kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo sekta ya afya, elimu na maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here