24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti Serikali ya Mtaa kizimbani kwa kuitukana Serikali

ERICK MUGISHA – DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Basihaya cha simba, Marinous Endule (39), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, kwa kuitukana Serikali.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Neema Moshi, alidai  Agosti 14, eneo la Basihaya cha simba wilayani Kinondoni, mtuhumiwa aliitukana Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kusema “hii Serikali ya kipumbavu imechoka, inakuja kwa wananchi kuiba pesa” na matumizi mengine ya lugha mbaya, kitendo ambacho kinaweza kusababisha uvunjaji wa amani.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Mwendesha Mashtaka Moshi alisema upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kesi kutajwa.

Hakimu Kiliwa alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua za utambulisho, nakala za vitambulisho na kusaini bondi ya Sh 1,000,000.

Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na yupo nje kwa dhamana. Kesi itakuja kwa kosomwa tena Septemba 27.

Wakati huo huo, watu watatu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Waliofikishwa mahakamani ni Samwel Daudi (26), mkazi wa Wazo, Juma Mohamed (31), mkazi wa Boko Chama na Brayan Yakobo (20), mkazi wa Boko Dawasco, Dar es Salaam.

Wakisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hellen, alidai Julai 2, eneo la Mbweni Malindi, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam washtakiwa walimuua Omary Yahaya.

 Alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ili kusikilizwa tena kesi hii.

Hakimu Mwakalinga alisema mahakama haina dhamana ya kuendesha kesi hiyo na washtakiwa wote hawatakiwi kujibu chochote hadi kesi itakapofika Mahakama Kuu.

“Washtakiwa wote mtakuwa mkitokea rumande kwa sheria na kanuni ya kosa lenu kutokuwa na dhamana, kesi yenu itakuja kwa kutajwa tena Septemba 7,”  alisema Mwakalinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles