25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MWENYEKITI GEITA ATIMULIWA KIJIJINI KWA ‘KUZUIA’ MVUA

rain-10

NA EMMANUEL IBRAHIM,GEITA 

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Lubanda Kata ya Busanda, Wialaya ya Geita kati ya mwaka 2009 hadi 2014 ya uongozi wake, Julius Petro, amefurushwa kijijini hapo yeye na familia yake baada ya wananchi kumtuhumu kuwa amezuia mvua isinyeshe.

Sakata la kutimuliwa kijijini hapo liliafikiwa na wananchi Novemba 25 mwaka huu katika mkutano wa hadhara ulioketi kujadili changamoto mbalimbali, ambapo miongoni mwa ajenda zilizozungumziwa ni mwenyekiti huyo wa zamani kudaiwa kuifunga mvua isinyeshe.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi juzi, Petro, alidai kuwa ameamua kukimbilia ofisi za mkuu wa wilaya ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo kwani familia yake haina amani kutokana na vitisho anavyovipata.

“Nimekuja kwenye ofisi za mkuu wa wilaya kuonana naye..nimefukuzwa kijijini mwenyekiti pamoja na wananchi wakinituhumu kuwa mimi ndiye nimesababisha mvua isinyeshe, familia yangu nimeitoa kijijini kwa kuhofia usalama wetu…nilitangazwa mimi ni mchawi nimezuia mvua kwenye kijiji hicho, kwa kweli nahofia maisha yangu na familia kwa ujumla,” alisema Petro.

Aidha, alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yalijadiliwa lakini alishangaa kuona mwenyekiti akiamuru wananchi kwenda kuvunja nyumba yake, lakini aliyekuwa amekaimu nafasi ya ofisa mtendaji wa kijiji ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi, hakumtaja jina aliwakataza wananchi kujichukulia sheria mkononi ndio ikawa ponapona yake.

“Lakini hatua zilizokuwa zimechukuliwa na wananchi ni kwenda kuvunja nyumba yangu na mimi nipigwe bahati nzuri kaimu ofisa mtendaji, mwalimu mkuu wa shule ya msingi, aliwazuia wananchi kufanya kitendo hicho…na siku hiyo walikubaliana kutekeleza agizo la mwenyekiti,” aliongeza Petro.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji aliyepo madarakani kwa sasa Elias Mlyamali, alipotafutwa na gazeti hili kutolea ufafanuzi wa jambo hilo, alikana kuhusika na kitendo hicho huku akikiri wananchi waliafikiana kutimuliwa kwa kiongozi huyo wa zamani.

‘’Kutokana na maneno hayo ndugu mwandishi, Julius Petro, amejiharibia mwenyewe asinitafute ubaya mimi wananchi walikuja kwenye mkutano na kusema maneno hayo…wenyewe wakiamini kabisa kuwa ni kweli amefunga mvua mwandishi ukiangalia na hali ya mvua ya mwaka huu kwanini wananchi wasiamini maneno yake walighadhibika,’’ alisema Mlyasmali mwenyekiti wa kijiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles