27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MWENYEKITI CCM AWAFUTA MACHOZI WAJANE

NA RAYMOND MINJA- IRINGA


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa,

Albert Chalamila, juzi ametoa kifuta machozi cha Sh milioni tatu kwa wajane

wawili na majeruhi mmoja wa Kijiji cha Makuka ambao mwishoni mwa mwaka jana, waume zao walidaiwa kuuawa na polisi katika operesheni ya kuondoa watu waliokuwa wakidaiwa kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo linalodaiwa ni hifadhi.

Eneo la Mundomela Magharibi, lililokaribu na kijiji hicho linaloelezwa ni la hifadhi ya jamii ambalo ni mapito ya tembo, limekuwa na mgogoro wa muda mrefu wa takribani miaka mitatu iliyopita bila ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mwenyekiti wa Kijiji hicho,

Habibu Nziku, alisema wananchi wamekuwa wakiishi maisha ya tabu na hofu, kwani wamekuwa hawana sehemu ya kulima baada ya kunyang’anywa maeneo yao na Serikali.

Alisema mgogoro huo ulianza mwaka 2016 ambapo walikuja watu na

kuanza kukata mazao ya wakulima na kuwafukuza watu kutokuendelea kulima katika maeneo hayo.

“Jambo la kushangaza mwaka 2007, alikuja ofisa utumishi hapa na

kundi kubwa la polisi na kutuambia nakwenda kuwaonyesha mipaka yenu na akatuambia mimi sitaki swali wala ushauri, ninachotaka twendeni

nikawaonyeshe mipaka na ambaye hataki  nitaenda kuwaonyesha

walioko tayari.

Alisema kwa juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Rihard Kasesela, walianza tena kufanya shughuli za kilimo lakini  hawakudumu.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Sofia Petro, mama wa watoto wa wawili ambaye ni mjane, aliyepoteza mume wake katika mgogoro huo, alisema amekuwa akiishi maisha ya tabu.

“Siku ya tukio nilikuwa nyumbani na mume wangu alikuwa ameenda

shambani, kumbe kulikuwa na polisi walikuwa wamekuja kuwaondoa

watu katika maeneo hayo, wakati wakiwa katika purukushani nasikia

polisi waliishiwa mabomu wakaanza kutumia risasi za moto na mojawapo ilimpata mume wangu na kupoteza maisha.”

Naye Veronika Sanga ambaye naye ni mama wa watoto wawili,

ambaye pia alimpoteza mumewe kwenye mgogoro huo, aliomba Serikali

kuingilia kati mgogoro huo ili wanakijiji hao waweze kupata

sehemu ya kulima ili kuwalisha watoto wao.

Kwa upande wake, Chalamila, alitoa siku saba kwa Kasesela kufika katika kijiji hicho ili kutafuta mwafaka wa kudumu wa mgogoro huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles