25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MWANZA WAZIRI AAGIZA WANANCHI WAPIMIWE ARDHI HARAKA

Na PETER FABIAN

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amewaagiza maofisa ardhi wa Manispaa ya Wilaya ya Ilemela kuacha kuwabagua baadhi ya wananchi katika   upimaji shirikishi na urasimishaji makazi kwa kisingizio cha kutokamilisha kulipia  gharama za upimaji ardhi.

Mabula ambaye ni Mbunge wa   Ilemela (CCM), alitoa agizo hilo  alipohudhuria kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilemela.

Aliwataka maofisa hao kuwapimia wananchi wote bila ubaguzi hata kama hawajakamilisha malipo kuondoa usumbufu  utakapozinduliwa mpango kabambe wa  Jiji la Mwanza.

“Wizara imeelekeza kupima kila kipande cha ardhi nchini, hivyo naomba maofisa ardhi wa Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kutekeleza hatua hii haraka.

“Hakikisheni  mmepima maeneo yote ya ardhi ya

wananchi kabla ya kuzinduliwa hivi karibuni mpango kabambe   ambao umelenga pia Mwanza kuwa   jiji la kisasa,”alisema.

Mabula alisema   baada ya kuzinduliwa   mpango huo hakutakuwa na upimaji ardhi shirikishi tena kwa utaratibu wa sasa.

Alisema kwa sababu hiyo ili wananchi wasilalamike ni vema wakapimiwa ardhi kwenye mitaa yao kabla ya

wizara kuuzindua rasmi mpango huo hivi karibuni.

“Wananchi wamenilalamikia kama mbunge kuwa wamekuwa wakirukwa na kubaguliwa kupimiwa na maofisa ardhi  kwa kisingizio kuwa hawajakamilisha uchangiaji fedha  urasimishaji makazi katika mitaa ya Ibungilo na Kiloleli.

“Hebu wapeni elimu kuwa waendelee kulipa hata kidogo kidogo hadi watakapomaliza siyokukataa kuwapimia,”alisisitiza.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Wanga aliahidi kulisimamia suala hilo lililojitokeza .

Alisema agizo hilo atalisimamia kwa kukaa na

wataalamu wake wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi   na kitengo cha upimaji kuhakikisha hakuna mwananchi atakayetoa malalamiko ya kutopimiwa eneo lake hata kama hayupo.

Naye Meya wa Manispaa hiyo, Renatus Mulunga (CCM) alisema ataangalia uwezekano wa kuwasamehe wazee wasiokuwa na uwezo  wa kuchangia gharama za upimaji shirikisi katika urasimishaji makazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles