30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAMKE ANAYEKULA KWA MIGUU, KUTEMBEA KWA MIKONO

JOSEPH HIZA Na MASHIRIKA

KWA kawaida binadamu wamejaliwa vipaji tofauti tofauti, ambavyo mara nyingi ili kuviendeleza, visipotee au ving’are zaidi mazoezi au mafunzo huhitajika.

Lakini ni hali tofauti kwa Leilani Franco (29), mkazi wa London, mwenye kipaji cha kuukunja, kuuzungusha na kuendesha shughuli kwa kutumia viungo visivyo husika.

Akiwa na uraia wa nchi mbili yaani Uingereza na Philippines Leilani anaweza kusafiri kwa namna mbalimbali umbali wa mita 20 katika muda wa dakika  10.05.

Rekodi hiyo aliiweka wakati aliposhiriki katika  tamasha la Royal Hall mjini London Uingereza, Machi 11, 2013.

Kutokana na uwezo wake huo wa kupinda atakavyo hasa kuelekea nyuma amebatizwa jina la backbend.

Pia kama inavyodhaniwa kwa kawaida mtu anaweza tumia mikono kwa kulia chakula na kufanya shughuli nyingine, katika hilo kwa mwanamke huyu pia ana upekee.

Yaani ana uwezo wa kutumia miguu yake  katika shughuli zake binafsi kama kula na kadhalika mikono akiitumia katika shughuli nyingine kama vile kutembelea.

Licha ya uwezo wake, anadai kwamba hula vyakula vya mafuta, hunywa vinywaji vya aina zote na kuvuta sigara wakati mwili wake ukibakia katika unyumbulifu.

Mtaalamu huyo wa sarakasi na viungo vya mwili anashikilia rekodi ya dunia ya kujikunja na kujizunguka kwa haraka zaidi.

Ni pale alipokuwa na umri wa miaka 18 wakati akiangalia kikundi cha sarakasi ndipo alipobaini vipaji vyake baada ya kujitosa kama utani kujaribu kuonesha alicho nacho wakati wa shoo ya kikundi hicho.

Amefanya maonesho sehemu mbalimbali duniani na uwezo wake wa kujikunja na kuuzunguka mwili atakavyo umempatia wafuasi wengi na daima hufurahisha watazamaji jukwaani ambao humpigia makofi.

Lakini tofauti na wanasarakasi wengine, ambao hutumia muda mwingi kufanyia mazoezi ili kujiweka sawa kuonesha uchawi wao, Leilani anayekula na kunywa chochote atakacho na hafanyi mazoezi.

Anasema: “kamwe sifanyi mazoezi ili kuwa na uwezo huu wa unyumbulifu ndivyo nilivyo.

“Makocha wangu raia wa Urusi huniambia kwamba ninapaswa kuzingatia mlo, nisinywe pombe au kuvuta sigara lakini ukweli napenda jibini, kuvuta sigara, kunywa pombe na vyakula vyenye mafuta.

Ushiriki wake wa nyuma kama mnenguaji ulimpa Leilani uzoefu unaohitajika kufanya onesho mbele ya umati mkubwa, lakini vipaji vyake hujidhihirisha kila  siku kutokana na uvumbuzi wa staili mpya anaouonesha.

Anaweza kula, kupaka rangi nywele na kuvuta sigara kwa miguu yake.

Anasema: “staili mpya kila siku kwa ajili ya kuvutia hadhila.

“Kwa mfano, nilikuwa nikipiga meno yangu mswaki kwa mikono na nikaone nifanye hivyo kwa miguu.”

“Najaribu kufanya kila kitu kwa miguu yangu au kichwa chini miguu juu kwa kadiri inavyowezekana ili tu kuona vitu kwa namna mpya.”

Ijapokuwa hakuna kati ya mbinu atumiazo zinazomuumiza, kinachoshangaza ni kuwa Leilani hupata ugumu wa kujikunya kuelekea mbele kwa sababu hutumia muda mwingi kujikunya kuelekea nyuma.

Wakati sarakasi anazofanya zikionekana kama za kuumiza, Leilani, ambaye aliingia nusu fainali ya shindano la vipaji Uingereza la Got mwaka 2012, hana mpango wa kuachana na kazi yake hiyo isiyo ya kawaida.

Anasema kwamba katika umri wake wa miaka 29 hajaona athari zozote bado.

“Sina majeraha kamwe sijawahi umia katika maisha yangu na sihisi dalili za kupunguza kasi.”

 

Kipaji cha Leilani kinamaanisha anaweza kutumia miezi mingi mbali na nyumbani lakini wazazi wake hawana wasiwasi.

Anasema familia yake inamuunga mkono kwa asilimia 100 kusafiri ng’ambo na kufanya maonesho.

“Nadhani wao pia wanajivunia – daima wamekuwa wakiona fahari kunikutanisha na marafki zao!”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles