27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanamkakati wa Maalim Seif aitwa kuhojiwa polisi Z’bar

eddyNA KHELEF NASSOR, ZANZIBAR

MWANAMKAKATI wa aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mohammed Ahmed Mugheiry, maarufu kama Eddy Riyami, jana aliitwa makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar kwa ajili ya kuhojiwa.

Riyami ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, alifika polisi kuitikia wito wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, SSP Simon Pasua.

SSP Pasua alimwandikia barua Riyami aliyekuwa katika Kamati ya Uchaguzi ya Maalim Seif Sharif Hamad, akimtaka kufika ofisi ya upelelezi iliyopo Makao Makuu ya Polisi Zanzibar bila kukosa jana saa 2 asubuhi.

“Kufika kwako ndiyo mafanikio ya wito huu, kuna mambo muhimu yanayokuhusu,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Lakini polisi waliahirisha wito huo dakika za mwisho hadi Jumatatu, huku Riyami akiwa tayari amefika ofisi ya upelelezi.

Akizungumza na MTANZANIA, Riyami alisema hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Kamishna Pasua kuitwa Dar es Salaam kwa shughuli za kikazi.

Alisema wito huo anautafsiri kuwa umeegemea zaidi katika masuala ya kisiasa, na kwamba hakuwa na sababu ya kutokwenda polisi kwa vile anaamini hana kosa lolote la uhalifu.

“Sikuona sababu ya kutokwenda kusikiliza wito, maana sina kosa lolote la uvunjifu wa sheria.

“Ninaamini yatakuwa ni masuala ya kisiasa, ingekuwa si masuala ya kisiasa ingekuwaje niitwe kwenye sehemu kubwa kama ile?” alisema Riyami.

Hata hivyo, alisisitiza kuripoti tena Jumatatu kama ilivyopangwa.

Katika hatua nyingine, Riyami alizungumzia uwapo wa vijana wanaofanya uhalifu wakiwa wamejifunika nyuso zao wanaofahamika katika visiwa hivyo kama ‘Mazombi’.

Riyami alilitupia lawama Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuwa na nia ya dhati ya kupambana na kundi hilo.

“Katika suala la Mazombi, namnyoshea kidole Kamishna Mkuu wa Polisi Zanzibar, ameshindwa kuchukua hatua stahiki za kupambana na kundi hilo ovu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles