Mwanafunzi akabidhiwa milioni zaidi ya 226.8 na m-bet

0
1727

Iman Mketema –Dar es Salaam

 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo Arusha, Meshack Daniel leo Desemba 1 amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni 226.8 baada ya kushinda mchezo wa Bahati Nasibu unaoendeshwa na kampuni mbili ya M-Bet na Perfect 12.

 

Meneja wa masoko wa M-bet, Allen Mushi, amemtangaza mshindi huyo huku akihamasisha watu wengine kucheza mchezo huo kwa kuwa wapo wengi walioshinda zaidi ya kiasi alichoshinda mwanafunzi huyo.

 

Mwanafunzi huyo amesema siku alipokwenda kubeti alitoka darasani kwao na kwenda kubeti kisha akarudi kuendelea na shughuli zake usiku akapokea meseji iliyomweleza ameshinda.

 

“Sikuwa na imani ya kushinda hadi leo nimepokea fedha ndiyo naamini, hata wazazi wangu hawajui hili swala nimeamua kuja mwenyewe kama mtoto wa kiume na nashukuru kweli nimeshinda,” ameeleza.

Kwa ligi ya England, Meshack anashabikia timu ya Manchester United, Hispania anashabikia Barcelona, Ujerumani anashabikia Bayern Munich na Italia anaishabikia Juventus.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here