Mwamunyange amuonya mkandarasi kuchelewesha mradi wa maji Chalinze

0
680

     Tunu Nassor, ChalinzeMwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Chalinze kukamilisha mradi huo kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.

Akizungumza  katika ziara ya kutembelea mradi huo, leo Alhamisi Oktoba 4, Mwamunyange amesema mradi huo umechelewa kukamilika kutokana na changamoto mbalimbali.

Amesema mkandarasi huyo ameongezewa muda wa kukamilisha mradi mara tatu lakini mpaka sasa hajakamilisha.

“Wametueleza changamoto zao lakini hatukubaliani nazo tunachotaka ni kukamilisha mradi huu hadi kufikia Disemba 31, mwaka huu,” amesema Mwamunyange.

Amesema hatua mbalimbali za kuuokoa mradi huo zimechukuliwa na serikali ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa akaunti maalumu ya fedha za mradi huo zinazotolewa na mfadhili kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi na upatikanaji wa vifaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here