24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MWALIMU MKUU ADAIWA KUTOWEKA BAADA YA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

                                                                   |Gurian Adolf, Nkasi



Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, kata ya Kala wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Eradi Kapyela ametoweka katika na kwenda kusikojulikana baada ya kudaiwa kumpa mimba mwanafunzi wake wa darasa la saba.

Taarifa hiyo ilibainishwa jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani baada ya Mbunge wa Nkasi Kusini, Desderius Mipata kualalamika ndani ya kikao hicho kuwa ameshangazwa na kitendo cha serikali kutomchukulia hatua  mwalimu huyo kwa kitendo hicho.

Amesema mimba kwa wanafunzi wilayani humo bado ni tatizo hivyo jitihada za makusudi za mapambano ni lazima ziendelee na kuwa mwalimu huyo ni lazima achukuliwe hatua za kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Missana Kwangulah amesema  taarifa za mwalimu huyo wanazo na juhudi za kumsaka zinaendelea kwani muda wa siku tano umepita tangu mwalimu huyo atoweke katika kituo chake cha kazi bila taarifa na kwaamba amefanya hivyo kukwepa mkono wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles