28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MWAKYEMBE KUFUNGUA TAMASHA LA 36 LA BAGAMOYO

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo litaanza keshokutwa katika viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni ya Bagamoyo (TaSUBAa), mjini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Dk. Herbert Makoye, alisema jumla ya vikundi 68 vimethibitisha kushiriki tamasha hilo mwaka huu vikiwemo vikundi kutoka nchi nane za Afrika na nje ya Afrika.

“Mgeni wetu rasmi katika ufunguzi tunatarajia atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na siku ya ufunguzi kutakuwa na matukio kadhaa ikiwemo maonyesho ambayo yataanza saa nane mchana hadi 11 jioni,” alisema Makoye.

Tamasha la mwaka huu limebeba kaulimbiu ya sanaa na utamaduni katika vita ya dawa za kulevya ambapo alisema wamechagua kaulimbiu hiyo kwa ajili ya kutoa elimu juu ya dawa za kulevya hapa nchini.

Alisema tamasha la mwaka huu limedhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Kamapuni ya New Habari (2006) Ltd, inayochapisha magazeti ya Bingwa, Dimba, Rai, Mtanzania na Mtanzania Digital, wadhamini wengine ni EFM, Tulia Trust, Azam Food Products, Azam TV,  TanTrade, Mlimani TV, Millenium Hotel,CRDB Bank, TBC, Ubalozi wa Ujerumani, Pepsi, Jumbo, Michuzi Blog, Basata na Kaya FM ya Bagamoyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles