25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MWAKYEMBE AVIMULIKA VYOMBO VYA HABARI VYA DINI

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amevitaka vyombo vya habari vya taasisi za dini nchini, kutoandika habari zinazopotosha jamii.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini kuhusu uzalendo kuelekea Tanzania ya viwanda.

Dk. Mwakyembe aliwataka viongozi hao wa dini kuhakikisha wanaendelea kuvilea vyombo hivyo ili visikiuke misingi ya uandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vinaelewa na kuzingatia sheria mbalimbali.

“Miongoni mwenu ni wamiliki wa vyombo vya habari, niwaombe muendelee kuvilea, japo si mara nyingi tumekuwa na malalamiko ya vyombo vyenu kuandika habari zinazopotosha, lakini vipo vichache vimewahi kuandika vibaya.

“Endeleeni kuongea na hivi vyombo na magazeti, Serikali inaheshimu sana uhuru wa vyombo vya habari katika kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa, lakini vizingatie sheria,” alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema ikiwa vyombo vya habari vitaendelea kuandika habari zinazopotosha wananchi, zinaweza kuvuruga amani hali itakayowafanya Watanzania wageuke kuwa wakimbizi badala ya wao kupokea wakimbizi.

“Msichoke kuhubiri amani, miaka 56 ya uhuru imetufunza mambo mengi, kwa sababu tumekuwa tukipokea wakimbizi kutoka DRC, Rwanda na nchi nyingine, mambo haya huanza polepole na hatimaye kuwa makubwa,” alisema Dk. Mwakyembe.

Aliwataka viongozi wa dini kuwasisitiza wananchi kulipa kodi, kufanya usafi na kuhifadhi mazingira, kufanya kazi kwa bidii, kuwa waaminifu, kuwajibika, kulinda rasilimali, kutii mamlaka, kupinga rushwa, dawa za kulevya na kuwa wazalendo.

Akizungumza katika mkutano huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema haiwezekani mtu akaishi katika taifa alafu halipendi taifa lake, hiyo ni dalili ya wazi kuwa mtu huyo si mzalendo.

Alisema suala la kupinga ufisadi na kufanya kazi si la rais pekee, bali ni la kila mwanachi mzalendo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles