24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MWAKINYO:LULU YA TANZANIA INAYONG’ARA KWENYE MASUMBWI

Na DINA ISMAIL-TUDARCo



Ushindi wa  Technical Knockout  (TKO), alioupata bondia  Mtanzania  Hassan Mwakinyo,  dhidi ya bondia Mwingereza  Sam Eggington, umekuwa gumzo kwa mashabiki wa mchezo  huo duniani.

Gumzo linatokana na mashabiki kutoamini kama Mwakinyo angeshinda, hasa kutoka na Eggington kuwa na rekodi nzuri zaidi, lakini matarajio yakawa tofauti.

Dalili za Mwakinyiko kushinda zilioneka wazi tangu raundi ya kwanza ya mpambano huo, ambao haikuchukua muda mrefu alipomtwanga makonde mfululizo mpinzani wake, huku raundi ya pili akiendeleza kumsukumiza makonde bila majibu, kabla ya mwamuzi Kevin Parker kumnusuru Eggington kwa kumaliza pambano.

Mwakinyiko (23) alimshinda Eggington (25) mwishoni mwa wiki iliyopita katika sekunde ya 45 ya raundi ya pili ya pambano lilisilo la ubingwa uzito wa kati lililofanyika katika Uwanja wa Arena Birmingham, mjini Birmingham, England.

Mpambano huo ulikuwa wa utangulizi kabla ya pambano kuu lililowakutanisha Amir Khan na Samuel Vargas, ambalo Khan alishinda kwa pointi.

Na Mwakinyo baada ya ushindi huo atapanda tena ulingoni Oktoba 20, kuzipiga na mwenyeji Wanik Awdijan Ukumbi wa Alex Sportcentrum mjini Nuremberg, Ujerumani, katika pambano la kuwania taji la vijana la IBF uzito wa Middle.

Pambano hilo lilikuwa la tatu Mwakinyo kupigana nje ya Tanzania, akiwashinda kwa mara ya pili baada ya kumshinda pia kwa TKO Anthony Jarmann wa Namibia Agosti 8, mwaka jana, ukumbi wa Grand Palm Hotel mjini Gaborone, nchini Botswana.

Na Mwakinyo baada ya ushindi huo wa jana atapanda tena ulingoni Oktoba 20, kuzipiga na mwenyeji Wanik Awdijan ukumbi wa Alex Sportcentrum, mjini Nuremberg, Ujerumani, katika pambano la kuwania taji la vijana la IBF uzito wa Middle.

Ushindi huo umemfanya Mwakinyo kujiamini zaidi, ambapo vyombo mbalimbali vya habari vilimnukuu akidai kwamba anamtaka Khan.

Desemba 2, mwaka jana, Mwakinyo alipoteza kwa pointi mbele ya mwenyeji, Lendrush Akopian ukumbi wa Krylia Sovetov mjini Moscow, Urusi.

Mwakinyo aliushangaza ulimwengu wa masumbwi kwa kumtandika Mwingereza Sam Eggington mwenye miaka 25 katika raundi ya pili, amesema yupo tayari kupambana na Khan.

Wakati Mwakinyo akiwa na rekodi hiyo, ameshinda mapambano 11 na kupigwa mawili, mpinzania wake alikuwa ameshinda mapambano 24 na kupigwa manne. Eggignton pia ni bingwa wa zamani wa Uingereza, Ulaya na nchi za Jumuiya ya Madola.

Mara baada ya ushindi huo, Mwakinyo alisikika akiimba kuwa anataka kupambana na bondia mwingine kutoka Uingereza, Kell Brook.

“Yeye (Eggington) aliingia ulingoni akiwa mwenye kujiamini sana. Nilitaka kuonesha uwezo wangu, sisi wengine ni mabingwa pia lakini hatuonekani kutokana na mzingira tunayoishi,” alisema Mwakinyo baada ya pambano hilo na kuongeza: “Nimefurahi sana kwa ushindi huu na nimeionesha dunia uwezo wangu halisi.

“Sasa nataka kupambana na Kell Brook na nikishamchapata namtaka Amir Khan.” Alipoulizwa kama wataweza kustahimili nguvu za Brook akajibu kwa kujiamini: “Kwani wanionaje?”

Bondia huyu wa Tanzania, wengi hawakuwa wakimfahamu, lakini uwezo wake kwa sasa umeanza kushangaza na kufuatiliwa na wengi kwenye medani ya masumbwi.

Mwakinyo anaweza kuwa lulu kwa kupeperusha vyema Bendera ya  Tanzania, iwapo Serikali itashirikiana naye katika kuhakikisha anafanya vizuri zaidi katika mapambano yake mengine yajayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles