30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mvua zawaacha bila makazi Rukwa

Na Gurian Adolf-Kalambo

KAYA 47 zimebaki bila makazi baada ya nyumba 13 kubomoka kutokana na mvua iliyonyesha juzi katika Kijiji cha Kasitu, Kata ya Sopa, Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya tukio  hilo, wakazi wa kijiji hicho walisema mvua hiyo ilikuwa kubwa  na iliyoambatana na upepo mkali.

Anold Yolam, mkazi wa  kijiji  hicho,  alisema baadhi ya watu ambao nyumba zao zimebomoka,  wamepewa hifadhi kwa  mwenyekiti  wa serikali  ya  kijiji na wengine  kwa majirani na kuiomba  Serikali iwasaidie.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Gasper Kateka, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimebomoka wamepewa hifadhi kwa  mwenyekiti wa kijiji  na wengine  kwa  majirani  wakati  wakisubiri  msaada  zaidi.

Mwenyekiti  wa  kijiji  hicho, John Sizo  alisema wananchi wengine ambao hawakupatwa na janga hilo wana wajibu wa kuwasaidia watu waliopatwa na maafa hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Just Binyura,  alisema tukio hilo limetokana  na wananchi kutojenga nyumba imara  na zenye  ubora.

Alisema nyumba nyingi zilizoathirika hazikuwa zimejengwa kwa kufuata taratibu za ujenzi, hivyo wananchi wanapaswa kuwashirikisha wataalamu wa  halmashauri ili wawape ushauri wa namna ya kujenga nyumba bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles