Muuza Chipsi ajitokeza kumtetea Zitto mahakamani adai amebaini hajafanya uchochezi

0
1436

Tunu Nassor -Dar es salaam

SHAHIDI wa upande wa utetezi wa kesi inayomkabili Kiongozi wa chama ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Musa Bakari (42) ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa licha ya kutofahamiana na mshtakiwa ameamua kutoa ushahidi baada ya kubaini maneno aliyoyatoa si ya uchochezi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, Bakari Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Boniface Mapunda alidai kutokana na maneno yaliyotamkwa kwenye hotuba kuishauri Serikali na Jeshi la Polisi juu ya usalama wa nchi aliona maneno hayo si ya uchochezi.Bakari ambaye ni mfanyabiashara wa chipsi amedai Oktoba 28, mwaka 2018 akiwa katika eneo lake la biashara Tandika jijini Dar es Salaam katika simu yake ya mkononi alimwona Zitto akizungumza na waandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamii.

Alidai kuwa katika taarifa hiyo Zitto alikuwa akizungumza mambo mbalimbali ikiwamo kumpongeza Samatta kwa kushinda goli pamoja na kuwapongeza wanaharakati.

“Mambo mengine aliyokuwa akiongea ni pamoja na suala la utekaji watu, kuuwawa kwa watu Kibiti na suala la mauaji yaliyotokea Kigoma ambapo alizungumzia watu kuondolewa kwa nguvu na wengine kuuawa na akaishauri Serikali namna ya kufuatilia.

 “Sikuwa na taswira yoyote zaidi ya kumpongeza Zitto kwa kuishauri Serikali na polisi kufanya uchunguzi,” alidai Musa

Akihojiwa na wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga kama aliwahi kufuatilia kijijini Mpeta ili kubaini mauaji hayo shahidi huyo alidai hakuwahi kufuatilia kwa kuwa haikuwa kazi yake.

Aidha alipoulizwa ni lini alianza kufuatilia kesi hiyo Mahakamani hadi kufikia hatua  ya kutoa ushahidi alidai baada ya mahakama kumkuta Zitto ana kesi ya kujibu .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here