29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MUSWADA DAWA ZA KULEVYA KUTIKISA BLW

Na Muhammed Khamis (UoI)

MKUTANO wa tisa kikao cha tano cha  Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), unatarajiwa kuvuta hisia kali kwa wananchi na viongozi wa Serikali kutokana na kuwasilishwa kwa hoja binafsi ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa Baraza hilo, Raya Issa Mselem alisema kikao hicho kinatarajiwa kuanza kesho.

Alisema kila mmoja, sasa ni shahidi juu ya jitihada zinazofanyika Tanzania Bara  za kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kuathiri kwa kiasi kikubwa makundi ya vijana.

‘’Kutokana na hali hii, huwenda wajumbe wa baraza hili kupitia Mohamed Said Mohamed wameiona ipo haja ya kuwasilishwa hoja ili kuwekwa sheria kali zitakazozuia matumizi ya dawa hapa Zanzibar,’’alisema Raya.

Alisema miswada  mingine itakayowasilishwa ni pamoja na muswada wa kufuta sheria ya nembo namba 1 ya mwaka 1985 na sheria ya Zanzibar nembo ya Serikali na wimbo wa Taifa wa Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles