31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Museveni kuwa Rais wa pili kumfuata JPM Chato

Mwandishi wetu

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, anatarajiwa kufanya ziara binafsi ya siku moja nchini leo ambapo atakutana na mwenyeji wake, Rais John Magufuli, aliyemapumzikoni nyumbani kwake Chato mkoani Geita.

Museveni atakuwa ni Rais wa pili kumfuata Rais Magufuli Chato, baada ya Julai 6, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kufanya ziara binafsi ya siku mbili nchini ambapo alitua Chato na kukutana na mwenyeji wake.

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilisema “Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kesho (leo) Jumamosi tarehe 13 Julai, 2019 atafanya ziara binafsi ya siku  moja hapa nchini.

“Rais Museveni atamtembelea Rais Dk John Pombe Magufuli kijijini kwake Mlimani katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Akiwa Chato, Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli.”

Katika ziara ya Kenyatta, aliyeondoka nchini Julai saba, yeye na mwenyeji wake walikubaliana maeneo mbalimbali ya kushirikiana kibiashara.

Taarifa ya Ikulu ilisema viongozi hao wametaka biashara baina ya nchi hizo ikuzwe zaidi na kujenga uwiano wa kibiashara wenye maslahi kwa pande zote.

Rais Magufuli alisema kwa kuwa Kenya imefanya uwekezaji mkubwa Tanzania ikilinganishwa wa Tanzania nchini Kenya, wamekubaliana kuwa kampuni za Kenya zijielekeza kuongeza thamani ya bidhaa kwa kuanzisha viwanda vitakavyosindika mazao na kuchakata bidhaa mbalimbali hapahapa badala ya kusafirisha malighafi kwenda Kenya.

Taarifa hiyo ilisema viongozi hao wamekubaliana, Kenya itanunua gesi ya Tanzania badala ya kuagiza kutoka nje ya Bara la Afrika kwa kuwa Tanzania imejaaliwa gesi nyingi, na kwamba wameagiza mawaziri wa Tanzania na Kenya kukutana na kujadili namna Kenya itavyonunua gesi hiyo.

Kuhusu ziwa Victoria ambalo kwa asilimia 51 lipo Tanzania na kwa asilimia 5 lipo Kenya, taarifa hiyo ilisema Rais Magufuli alisema wamekubaliana kuwa mawaziri wa nchi hizo wahakikishe meli za Tanzania na Kenya zinaimarishwa na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha meli hizo kufanya kazi ya kukuza biashara katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambazo zinazunguka ziwa hilo.

Taarifa hiyo ilisema kwa upande wake Rais Kenyatta, alisema pamoja na kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya, wamekubaliana kuhakikisha nchi hizo zinakuwa na amani na kuheshimu mkataba wa kukabiliana na uhalifu.

Alisema Mtanzania atakayekamatwa kwa uhalifu nchini Kenya atashughulikiwa sheria za Kenya na Mkenya atakayekamatwa kwa uhalifu Tanzania, atashughulikiwa kwa sheria za Tanzania.

Ilisema Kenyatta alisisitiza kuwa Wakenya na Watanzania hawana sababu ya kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi bali kuhakikisha uchumi unakua, biashara inaongezeka na uhusiano na ushirikiano katika maeneo mbalimbali unaimarika zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles